Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta amesema anataka kufanya mdahalo na mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa ili aweke wazi ukweli kuhusu sakata la Richmond lililopelekea mgombea huyo kujiuzulu nafasi ya uwaziri mkuu mwaka 2008.

Sitta aliyasema hayo juzi katika uzinduzi wa kampeni za ubunge mkoani Shinyanga, ambapo alisisitiza kuwa Lowassa alihusika moja kwa moja na ufisadi mkubwa uliolisababishia hasara taifa.

Alisema kuwa Lowassa na wenzake walifanya njama ya ufisadi huo kwa kuunda kampeni hewa ya Richmond na Dowans zilizokuwa zikilipwa fedha nyingi za umma kwa ajili ya kufua umeme, kazi ambayo haikufanyika.

“Wakati wanaishari serikali, kumbe wao tayari wamekwishaunda kampuni nyingine hewa inaitwa Dowans, na Dowans hadil leo bado inatutafuna,” alisema Sitta. “Na deni la Dowans linatosheleza kujenga sekondari 23, na kila sekondari ya shilingi bilioni 3,”aliongeza.

Alieleza kuwa kitendo kilichofanywa na Lowassa na wenzake katika sakata hilo ni aibu kubwa kwa taifa hasa wanapotaka kupotoshwa ukweli hivi sasa huku wakiomba ridhaa ya wananchi kuwa viongozi.

Sita ambaye alikuwa Spika wa Bunge aliyeunda kamati maalum ya bunge iliyokuwa chini ya uenyekiti wa Harison Mwakyembe kuchunguza sakata la Richmond, iliyobaini ufisadi mkubwa kupitia kampuni hiyo yakufua umeme iliyobainika kuwa ‘kampuni hewa’, aliomba afanye mdahalo na Lowassa wiki hii ili aweke mambo bayana.

“Kama kweli yeye anasema hana hatia kuhusu Richmond, naomba wiki ijayo kuwe na mdahalo kwenye Star TV, Mwakyembe, mimi, yeye na rafiki zake wote atakaopenda kuwaleta. Taifa litusikilize na tuje na vielelezo,” Sitta alisema.

Zitto awashukia Ukawa, CCM kwa Ufisadi
ACT- Wazalendo Kuzindua Kampeni Zake Leo