Baada ya kukamilisha taratibu za kuajiriwa na kutambulishwa na Uongozi wa Young Africans, Kocha mpya wa makipa wa klabu hiyo Razack Siwa amewatuliza mashabiki na wanachama, kwa kusema ubingwa utatua Jangwani msimu huu 2020/21.

Siwa aliyewahi kuifundisha Young Africans miaka ya nyuma, amesema alikuwa akiifuatilia timu hiyo akiwa kwao Kenya, na ameona mabadiliko makubwa kuanzia kwenye kikosi tofauti na walikotoka.

Amesmea jambo kubwa ambalo linapaswa kufanywa klabuni hapo ni umoja na mshikamano kwa wachezaji, viongozi, wanachama na mashabiki ambao wana kiu ya kuona taji la Ligi Kuu linatua Jangwani.

“Muhimu kwa Young Africans ni kuhakikisha haipati sare wala kupoteza mchezo bali tunatakiwa tushinde michezo yote iliyobaki, hiyo itatupa nafasi ya kuchukua taji, lakini hili halitofanikiwa kama hatutakuwa pamoja.”

“Nilikuwa nikifuatilia michezo yote ya Young Africans waliyocheza, ni timu nzuri kuanzia wachezaji wa ndani hadi makipa, imeboreshwa kwa kweli sio ile ya wakati wa nyuma.”

“Nina imani kubwa nitarekebisha safu ya makipa, nilikuwa nafuatulia michezo yote nimeona baadhi ya makosa yao,” amesema.

Siwa amesema amefurahi pia kuona mazingira ya kambi ya kikosi cha Young Africans namna yalivyo mazuri na tulivu, huku akisisitiza yamemekaa kimpira na anayafananisha na maeneo mengine alikowahi kutembelea.

Historia kuandikwa AFCON 2021
Mambo yamenoga Ihefu FC