Imeelezwa kuwa maboresho ya miundombinu ya skimu ya kilimo cha umwagiliaji ya Igomelo iliyopo wilayani Mbarali Mkoani Mbeya, imewanufaisha kwa namna mbalimbali wakulima wanaojishughulisha na kilimo cha mbogamboga.
Hayo yamesemwa na Mhandisi wa kanda ya Mbeya wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Elibariki Mwendo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea skimu hiyo.
Amesema kuwa, Serikali imetumia kiasi cha shilingi Milioni miambili hamsini (250) kukarabati miundombinu ya skimu hiyo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa banio kubwa linalotoa maji katika chanzo cha maji cha mto Mbarali na mifereji inayopeleka maji mashambani.
“Katika skimu hii wakulima wanajikita zaidi katika kilimo cha mbogamboga kama vile Vitunguu, Nyanya, Matango, na hata zao la Mpunga, ambapo kabla ya marekebisho na maboresho ya miundombinu hii, hali haikuwa nzuri kwani wakulima walikuwa wanajichotea maji kiholela ili kuweza kumwagilia mazao yao, lakini kwasasa kama mnavyoona, maji yanakwenda mojakwamoja mashambani kwa utaratibu maalumu,” amesema Mwendo
Aidha, mmoja wa wakulima wanaojishughulisha na zao la kilimo cha vitunguu katika skimu hiyo. Yohana Mbuna (52) amesema kuwa amekuwa akijishughulisha na kilimo katika skimu hiyo kwa takribani miaka ishirini sasa.
Kwa upande wake Afisa Kilimo na Umwagiliaji kandaya Mbeya, Mnadi Taribo amesema kuwa kupitia Mradi wa kuwajengea uwezo wataalam na wakulima Tanzania Capacity Building for Irrigation Development (TANCAID) wakulima wameweza kupata Elimu kuhusu mafunzo na matumizi sahihi ya maji katika kilimo hususani kilimo cha mpunga kitaalam kilimo shadidi, usimamizi bora wa maji na kanuni sahihi za kilimo.
-
Flyover nyingine kubwa, yaanza kujengwa Dar
-
Prof. Mbarawa azindua mradi mkubwa wa maji
-
Video: Mo Dewji aibua shida mpya, Waziri apinga ripoti ya polisi
Hata hivyo, imeelezwa kuwa kanda ya kilimo ya Mbeya inayojumuisha mikoa ya Mbeya, Iringa, Njombe na Songwe ina jumla ya ukubwa wa hekta laki 268,350 ambapo Hekta 66,974 zimeendelezwa na Hekta 201,376 hazijaendelezwa na zipo kwenye mpango kabambe wa kitaifa wa kuendeleza kilimo cha umwagiliaji unaolenga kuendeleza hekta milioni moja (1,000,000,) katika awamu ya kwanza ya 2020 mpaka 2025 na awamu ya pili ya 2025 – 2035.