Kiungo Mshambuliaji kutoka Afrika Kusini, Mahlatse Makudubela ‘Skudu’ amewatoa hofu Wanachama na Mashabiki wa Young Africans na kuwaahidi kufanya vyema kwenye michuano ya Ngao ya Jamii, jijini Tanga.

Young Africans ambao ni mabingwa watetezi wa taji hilo watafungua dimba na Azam FC Uwanja wa CCM Mkwakwani, Tanga na baadae mchezo wa mchezo huo atacheza na mshindi kati ya Simba SC na Singida Fountain Gate Fainali.

Skudu aliyesajiliwa na Young Africans akitokea Marumo Gallants ya Afrika Kusini amesema wanafanya jitihada kwenye mazoezi ya timu hiyo kuhakikisha wanakwenda kufanya vizuri Tanga.

Akizungumza kambini Avic Town, Skudu amesema lengo lao ni kunyakua taji hilo ambapo ni lazima waitoe Azam FC kwenye mashindano hayo.

“Tunafanya mazoezi kwa bidii tukijua mbele yetu kuna mashindano ya Ngao ya Jamii, kipaumbele chetu ni kufanya vizuri na hivyo ni lazima tuwafunge Azam FC,” amesema winga huyo mwenye ufundi mwingi mguuni.

Amesema anajua michuano hiyo itakuwa migumu lakini wamejiandaa kimwili na kiakili kutetea ubingwa wao.

Gamondi: Mashabiki tulieni, tupo vizuri
Jeshi laungana na Wananchi kusherehekea, kutetea uhuru