Mmiliki wa Klabu Bingwa Duniani Chelsea FC, Roman Abramovich imeripotiwa kuwa yupo sawa baada ya kutajwa kuwa na dalili za maumivu katika macho, huku ikitajwa kuwa ni sumu za kemikali.

Kwa mujibu wa ripoti za uchunguzi wa mtandao wa Bellingcat, Abramovich na Ukraine walikuwa katika mazungumzo ya masuala ya amani alikuwa akisumbuliwa na maumivu ya macho.

Sky Sports imeripoti kwamba Abramovich yupo sawa na maisha yake hayapo katika hatari.

Bellingacat walitweet:”Bellingcat inaweza kueleza kuwa watu watatu ambao walikuwa katika kikao cha mazungumzo ya amani kati ya Ukraine na Urusi usiku wa Machi 3 na 4,2022 wameonesha dalili ambazo zinaonyesha kwamba wamepata sumu za kemikali.

“Miongoni mwa waathirika ni Mjasiriamali wa Urusi Roman Abramovich.”

TBS yawafikia wadau wa sekta ya utalii
Hassan Dilunga ndio basi tena Simba SC