Kiungo kutoka England Emile Smith Rowe huenda akawa chaguo la kwanza kwa Kocha Mikel Arteta kushika namba tisa ya Arsenal, baada ya Gabriel Jesus kukabiliwa na majeraha.

Arsenal wataanza msimu huu wakiwa finyu katika safu ya ushambuliaji, huku Gabriel Jesus akitarajiwa kukosekana kwa majuma kadhaa kutokana na majeraha.

Arteta alithibitisha habari hizo baada ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil kukaa nje kwenye mchezo wa juzi Jumatano wa Kombe la Emirates dhidi ya Monaco.

Eddie Nketiah na Folarin Balogun ni washambuliaji wengine kwenye vitabu vya timu hiyo ya London, huku Leandro Trossard akiingia kwenye nafasi hiyo mara kwa mara msimu uliopita.

“Nadhani anaweza kucheza katika nafasi nne,” Arteta alisema kuhusu Smith Rowe mnamo 2022.

“Kama winga wa kushoto, kiungo mshambuliaji wa kushoto, kiungo mshambuliaji wa kulia na anaweza kucheza kama tisa, vizuri sana.”

Smith Rowe alitumiwa kwa kiasi kidogo na timu yake ya utotoni msimu uliopita, kabla na baada ya matatizo ya kinena ambayo yalimfanya akose kucheza mwanzoni mwa msimu.

Alicheza mechi 12 pekee kwenye ligi, zote akitokea benchi, huku Gabriel Martinelli akipendelea nafasi ya upande wa kushoto ambayo Muingereza huyo alikuwa akicheza mara kwa mara msimu uliopita.

MAKALA: Madaraka ya kulevya Ikulu
Ally Kamwe awaita mashabiki Tanga