Kada wa zamani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Sofia Simba amerejeshwa ndani ya chama hicho miezi kadhaa baada ya kufukuzwa kwa usaliti.

Mama Simba ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake -CCM (UWC), amerejeshwa baada ya kuomba msamaha.

Uamuzi huo umefikiwa leo katika Mkutano wa Kamati Kuu (NEC-CCM), baada ya Mwenyekiti wa chama hicho, Rais John Magufuli kusoma barua yake ya kuomba msamaha na kuwahoji wajumbe wa kikao hicho.

“Mwanachama wa CCM aliyefukuzwa uanachama amekuwa akituandikia barua nyingi za kuomba msamaha, lakini tumekuwa tukikaa kimya, kwa sababu kikao hiki ndicho kilichomfukuza,” alisema Rais Magufuli.

 

Wajumbe waliridhia maombi hayo na kumkaribisha upya ndani ya chama hicho.

Sofia Simba alifukuzwa uanachama na kikao cha NEC baada ya vuguvugu la Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, baada ya kukutwa na hatia za kuwa msaliti kwa kuwasiliana na kambi ya mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa wakati wa kampeni.

JPM awafunda Msando na Masha
Sophia Simba arejeshwa kundini