Kiungo mpya wa Manchester United, Sofyan Amrabat amelazimika kujiondoa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Morocco kufuatia kuripotiwa kupata mjeraha huku akiwa ni muda mfupi tu, tangu akamilishe dili lake la kujiunga na Manchester United.
Manchester United ilikamilisha usajili wa Sofyan Amrabat siku ya mwisho ya dirisha la usajili ambapo taarifa za Unied kumfukuzia staa huyo wa Morocoo zilianza mapema baada ya kufunguliwa kwa dirisha la usajili.
Kiungo huyo wa kati wa Morocoo aliungana United kwa mkopo wa awali wa msimu mzima kutoka Farentina siku ya mwisho, huku Red Devils wakilipa timu hiyo ya ltalia ada ya mkopo ya Pauni Milioni 8 huku kukiwa na chaguo akufanya mkataba huo kuwa wa kudumu kwa Pauni Milioni 21 msimu ujao.
Amrabat alijipatia umaarufu mwishoni mwa mwaka jana alipokuwa sehemu muhimu ya mbio za kukumbukwa za Morocco hadi Nusu Fainali ya Kombe la Dunia, huku wakiwa timu ya kwanza kabisa ya Kiafrika kutinga hatua ya nne bora ya Fainali ya michuano hiyo.
Morocco ‘Simba wa Atlas’ wanatarajia kucheza dhidi ya Liberia mchezo wa kufuzu na baadae leo Jumamosi (Septemba 09) kuvaana na Burkina Faso ambao ni mchezo wa kirafiki.
Ukali wa jeraha la Amrabat bado haujafichuliwa, ingawa The Athletic iliripoti mapema juma hili jinsi United walivyogundua tatizo la mgongo wakati wa matibabu yake.
Hata hivyo, suala hilo halifikiriwi kuwa zito na wanataraja kumrejesha mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 katika utimamu kamili haraka iwezekanavyo.
Akizungumzia kujiunga kwake na United mapema juma hili, Amabat alisema: “Nadhani United walikuwa na wachezaji wengi wazuri na viungo wa kati, hivyo kwa ujumla, ninaangalia zaidi viungo, kama Paul Scholes, Roy Keane, David Beckham. Lakini kulikuwa na wachezaji wengi wakubwa kama Gary Nevlle, Rio Ferdinand, Louis Saha, Wayne Roney. [Cristiano] Ronaldo. Ninaweza kuendelea kwa saa moja kusema majina.”