Kiungo wa Fiorentina, Sofyan Amrabat analazimisha kuondoka ili akajiunge na Manchester United kabla ya dirisha la usajili kufungwa Septemba Mosi.

Kwa upande wa mabosi wa Fiorentina wanatarajia kupokea ofa nono, huku Man United ikihusishwa na nyota huyo wa kimataifa wa Morocco.

Ten Hag bado anataka kuongeza kiungo mkabaji baada ya kumuuza Fred.

Amrabat ameonyesha nia ya kwenda Old Trafford, lakini anasubiri makubaliano binafsi ya klabu hizo mbili ili kukamilisha uhamisho wake wa kuichezea timu hiyo ambayo ni mabingwa wa kihistoria wa Ligi Kuu England.

Man United imeonyesha kiwango kibovu katika mechi mbili za mwanzo wa Ligi Kuu England ambazo zimeianika Safu ya kiungo inayoonekana kupwaya, hivyo usajili wa Kiungo unahitajika haraka na Amrabat akipendekezwa.

Kiungo huyo alionyesha kiwango bora katika fainali za Kombe la Dunia na alikuwa nyota wa mchezo wa nusu fainali dhidi ya Ufaransa, licha ya kufungwa bao 1-0.

Wakati huo huo, gazeti la Per Corriere dello Sport limeripoti kwamba Amrabat anataka kujiunga na Man United tu akaungane na Ten Hag ambaye aliwahi kumnoa nchini Uholanzi.

Ten Hag na Amrabat wana mahusiano mzuri, lakini Man United inakabiliwa na ishu za kiuchumi na dili hilo linaweza kukwama kwani zimebaki siku chache kabla ya dirisha la usajili kufungwa.

Na sasa kutokana na uhamisho wa Amrabat kusuasua, kuna uwezekano Fiorentina ikamtoa kwa mkopo huku kukiwa na kipengele cha kumnunua.

Wakati huo huo kiungo huyo ameondolewa katika kikosi cha Fiorentina na hatacheza mechi hadi ishu yake ya usajili itakapopatiwa ufumbuzi.

Mancini akabidhiwa fupa jipya
Kikokotoo: Wabunge waanza upya Dodoma