Mshambuliaji kutoka nchini Hispania Roberto Soldado, anakaribia kuondoka jijini London nchini Uingereza kufuatia mipango iliyoweka hadharani na wakuu wa klabu ya Tottenham Hotspurs, ya kutaka kukiboresha kikosi chao.

Soldado, ambaye mpaka sasa ameshaifungua mabao saba Spurs tangu aliposajiliwa mwaka 2013, amekuwa na wakati mgumu wa kufikia malengo yaliyokuwa yamekusudiwa baada ya hali kuwa tofauti.

Ripoti zinasema kwamba huenda mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 30, akarejea nchini kwao Hispania baada ya uongozi wa klabu ya Villareal kuonyesha nia ya dhati ya kutaka kumsajili kwa kiasi cha paund million 11.

Hata hivyo mipango ya mshambuliaji huyo kutaka kusajiliwa na klabu ya Villareal huenda ikavurugwa na klabu ya Sevilla ya nchini Hispania pamoja na Benfica ya nchini Ureno, ambazo zimeonyesha utayari wa kumuwania Soldado.

Endapo Soldado atakamilisha mipango ya kuondoka Spurs katika kipindi hiki, atakua mchezaji wa nne ambaye alisajiliwa kutokana na fedha za manunuzi ya Gareth Bale, kuruhusiwa huko kaskazini mwa jijini London.

Wengine waliofunguliwa mlango na kuondoka White Hart Lane baada ya kusajiliwa kwa fedha iliyotokana na kuuzwa kwa Gareth Bale ni Paulinho, Etienne Capoue pamoja na Vlad Chiriches.

Rapa wa Kike Amvaa Nicki Minaj
Mourinho Aeleza Sababu Za Kuigawa Medali Yake