Aliyekua Meneja wa Msnchester United Ole Gunnar Solskjaer ana mpango wa kurejea katika majukumu yake ya ukocha huku akihusishwa na klabu ya Club Brugge ya Ubelgiji.

Klabu hiyo inatafuta kocha mpya kwa zaidi ya mwezi mmoja baada ya kumfukuza aliyekua kocha wake Scott Parker mwezi uliopita kutokana na mwenendo mbaya wa timu hiyo.

Kocha huyo wa zamani wa Fulham na Bournemouth alichukua nafasi ya Carl Hoefkens Julai mwaka jana, lakini katika mechi 12 alizoongoza msimu huu Brugge imepata ushindi mmoja tu.

Solskjaer alikuwa nje ya dimba tangu atimuliwe Manchester United Novemba 2021, mwezi mmoja tu ukiwa umebaki atimize miaka mitatu ndani ya Old Trafford.

Kwa mujibu wa mwandishi wa habari Sacha Tavolieri, jina la Solskjaer limependekezwa.

Kocha msaidizi wa FC Bayern Munich, Dino Toppmoller naye ameingia kwenye kinyang’anyiro cha kuwania ukocha Brugge baada ya kufukuzwa kazi, sabamba na Julian Negelsmann mwisho mwa mwezi uliopita.

Brugge ilivumilia nyakati ngumu walizopitia na sasa imedhamiria kusaka kocha mpya ambaye ataiweka timu kwenye mstari baada ya kuboronga msimu huu. Brugge iliondolewa raundi ya 16 bora ya Ligi Mabingwa Ulaya dhidi ya Benfica Februari mwaka huu na kuweka rekodi mbovu zaidi tangu miaka 16 iliyopita.

Rungu la adhabu laishukiwa Juventus FC
Ujenzi barabara kurahisisha usafirishaji, utoaji wa huduma