Maelfu ya wananchi nchini Somalia wameadhimisha mwaka mmoja wa siku nyeusi, siku ambayo ni kumbukumbu ya mauaji ya watu zaidi ya 580 kwa wakati mmoja yaliyotekelezwa na kikundi cha Kigaidi cha Al-shabab kwa kulipua bomu.

Mauaji hayo yalitekelezwa Oktoba 14 mwaka jana, huku serikari ya nchi hiyo ikaipa jina siku hiyo kuwa ni “black day”na kuweka kumbukumbu katika makutano ya barabara kwa jina la ‘Oktoba 14 junction’ kama kumbukumbu ya heshima kwa waliopoteza maisha.

Aidha, Meya wa mji wa wa Mogadishu ambao watu walikusanyika kuenzi siku ya mauaji hayo, Abdrahman Omar Osman. amewaambia wananchi kuwa kukusanyika kwao kwa wingi ni ishara kuwa ugaidi haukubaliki katika jamii ya Wasomalia, kwani licha ya siku hiyo kuwa ya majonzi bado imeweza kuwaunganisha watu kutoka sehem mbalimbali.

Kwa upande wake Waziri mkuu wa nchi hiyo, Hassan Ali Khaire amesisitiza kuwa shambulio hilo limefeli kuharibu  roho za Wasomali.

 

Hata hivyo, zaidi ya familia 225 zilipoteza watu wao katika shambulio hilo, huku zaidi ya watoto 1500 waliachwa yatima na kuna baadhi ya watu wengine hawakuonekena tena hivyo ikabidi wachukuliwe kama walikuwa miongoni mwa walio fariki katika shambulio hilo.

Kanye amzawadi kiatu Museveni
Kanye West akutana na Rais Museveni, ampa zawadi