Serikali ya Somalia imetangaza kufuta sherehe na shamrashamra za sikukuu za ‘Krismas’ nchini humo ikihofia mashambulizi ya magaidi wa Al Shabaab.

Mkurugenzi Mkuu wa Wizara inayoshughulikia masuala ya kidini nchini humo, Sheikh Mohammed Khyairo alisema kuwa marufuku hiyo imetolewa kutokana na kuwepo tishio la mashambulizi ya Al Shabaab kwa kuwa sherehe hiyo ni ya dini isiyo ya kiislamu.

Sheikh Mohammed amewaagiza maafisa wote wa usalama kuzuia na kuvunja mikusanyiko yoyote yenye nia ya kusherehekea sikukuu ya Krismas.

Mwaka jana, wanamgambo wa Al Shabaab waliovamia na kushambilia kambi za wanajeshi wa Umoja wa Kimataifa wakati wanajeshi hao walikuwa wakisherehekea Christmas.

Wanajeshi wa tano waliuwawa katika shambulio hilo.

Sitta amfuata Dk. Slaa, apiga chini siasa
Rais Apiga Marufuku Safari za Ndege Daraja la Kwanza kwa Watumishi wa Umma