Serikali ya Somalia imesema imemuita nyumbani Balozi wake nchini Kenya, Mohamud Ahmed Nur Tarzan, ikiishutumu nchi hiyo kwa kuingilia siasa za nchi yake na kumtaka balozi wa Kenya nchini Somalia kufunga virago kwa kile walichosema ni “kwa ajili ya majadiliano”.

Somalia imeishutumu Kenya kwa kushinikiza serikali ya Jubbaland kukataa makubaliano ya uchaguzi yaliofikiwa Septemba 17, katika uchaguzi mkuu ujao utakaofanyika mwezi ujao.

“Serikali ya Somalia ilichukua uamuzi huo kulinda eneo lake la utawala baada ya kujitokeza kuwa Kenya inaingilia kimakusudi masuala ya Somalia eneo la Jubbaland,” amesema Mohamed Ali Nur, Waziri wa Mambo ya Nje wa Somalia.

“Serikali ya Somalia imeonesha kusikitishwa kwake na serikali ya Kenya kwa kuingilia moja kwa moja masuala ya ndani ya siasa za Somalia hatua ambayo inaweza kuchangia ukosefu wa uthabiti, usalama na maendeleo kwa eneo zima,” ameongeza.

Kenya inaunga mkono utawala wa, Ahmed Mohamed Islam maarufu kama “Madobe” huko Jubbaland, kwa sababu ya maslahi yake ya kiusalama na kieneo.

Prof. Kabudi akutana na mabalozi wa China, Sweeden na Finland
Maafisa mawasiliano Ikulu ya Marekani watajwa