Serikali nchini Somalia imethibitisha kuwa imewatuma madaktari 20 kwenda nchini Italia ili kusaidia kuongeza nguvu ya mapambano dhidi ya virusi vya covid 19 vilivyoua watu 10,779 nchini humo huku kwa siku ya jumapili vikitokea vifo 756 na jumamosi vifo 889.
Msemaji wa serikali nchini Somalia, Ismail Mukhtar amesema madaktari waliotumwa ni wanaojitolea kutoka chuo kukuu cha chaifa ” The Somali National University” ambao tayari wamewahi kutembelea nchi za ulaya.
” Madaktari 20 tayari wamesajiliwa italia na wanatarajiwa kushirikiana na madaktari wengine kutoka ulimwenguni kote kuisaidia Italia kuhudumia waathirika wa virusi vya corona” Amesema Said
Aidha amebainisha kuwa madaktari hao wametumwa kama sehemu ya mwitikoa wa dharula kufuatia ombi la serikali ya Italia la msaada wa kimataifa wa madaktari.