Serikali ya Somalia imetangaza kusitisha uhusiano wake na Kenya ikidai kwamba Serikali ya Kenya inaingilia kati masuala yake ya ndani.

Nchi hiyo jirani ya Kenya, imetangaza kuwafukuza wanadiplomasia wote wa Kenya na kuagiza wanadiplomasia wake wote walio Nairobi kurudi Mogadishu ndani ya siku saba kuanzia leo Jumanne Desemba 15, 2020.

Waziri wa Habari wa Somalia, Osman Abubakar Dubbe, amesema katika hotuba iliyorushwa moja kwa moja na televisheni ya serikali ya Somalia Desemba 14,2020 kuwa hatua hiyo imechukuliwa kujibu uchokozi wa kisiasa wa kila mara unaofanywa na serikali ya Kenya kinyume na uhuru wa Somalia.

Hata hivyo Serikali ya Kenya haijajibu madai wala hatua hiyo ya Somalia.

Somalia ilimuondoa Balozi wake nchini Kenya Novemba 29 na kuamuru balozi wa Kenya kuondoka Mogadishu.

Guardiola: Arteta anahitaji muda
Koeman: Tunawaheshimu PSG, hatuwaogopi