Takribani shule 1000 nchini India, mji wa Delhi wameanzisha somo jipya ambapo wanafunzi watafundishwa somo la furaha linalochukua dakika 30 hadi 45 kila siku.

Somo hili hufundishwa kwa watoto waliopo elimu ya msingi na limeanza rasmi wiki chache zilizopita.

Ambapo wanafunzi hugawanywa katika makundi matatu na kisha kupewa kazi zinazosaidia kuwajenga kiakili.

Hadithi mbalimbali huhadithiwa katika vipindi hivyo, hali inayoboresha hali ya kiroho ya mwanafunzi.

Ni matumaini ya taifa hilo kuwa masomo hayo ya furaha yatawasaidia watu wengi kuishi maisha yasiyokuwa na msongamano wa mawazo na huzuni.

”Tumetoa wazalishaji bora viwandani, na tunaweza sema tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa. Lakini pia tumedhamiria kuwa na watu bora katika jamii na taifa kwa ujumla kwa kuanzisha darasa la kufundisha furaha” amesema Waziri wa Elimu wa India, Manish Sisodia.

Hata hivyo tayari matokeo chanya ya somo hilo la furaha yameanza kuakisiwa kwani kwa kiasi cha asilimia 65 matendo ya ukorofi kwa wanafunzi yamepungua, na asilimia 40 ya msongo wa mawazo pia umepungua sasa wanafunzi hujiamini, ubunifu na furaha vimeongezeka maradufu na kuchochea tabia njema baina yao na wakubwa wao.

Mwanafunzi mmoja wa Delhi mwenye umri wa miaka 11 katika kipindi cha furaha alisimama  na kusema kuwa ” Inatakiwa tufanye kazi kwa furaha, sababu ukiwa unafanya kazi kwa huzuni, chuki kazi yako haitakuwa nzuri na yenye weledi”.

 

Breaking: Basi lililobeba abiria 60 lateketea kwa moto Kigoma
Video: Kauli ya Nape yaibua upya hoja mgombea binafsi, Maagizo 12 ya Lugola