Mshambuliaji kutoka Korea Kusini Son Heung-min amemshukuru nahosha wa Tottenham Hotspurs Harry Keane, kwa kufanikisha ushindi wa mabao mtano kwa mawili dhidi ya Southampton, kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England uliochezwa jana Jumapili, Septemba 20.

Katika mchezo huo Son alifunga mabao manne pekee yake, huku bao la tano likifungwa na nahodha na mshambuliahi Harry Kean.

Mabao yote manne yaliyofungwa na mshambuliaji huyo, yaliwezeshwa kwa pasi za mwisho za Harry Kane.

Son amesema ushirikiano na uwajibikaji katika muda wote wa mpambano huo uliounguruma White Hart Lane baina ya wachezaji wote wa Spurs, ndio ilikua chanzo na siri ya mafanikio ya alama tatu walizozipata.

“Ninafuraha sana kufunga mabao manne kwa mara ya kwanza katika Premier League,” Son alisema katika ujumbe aliowekwa kwenye ukurasa rasmi wa Twitter wa klabu ya Spurs.

“Shukrani za dhati ziende kwa wachezaji wenzangu ambao wamenitengenezea nafasi za kufunga haswa kwa Harry Kane. Harry alikuwa katika kiwango cha ajabu sana, pasi za safi.”

“Kufunga hat-trick yangu ya kwanza katika Premier League nikiwa na Spurs ni heshima kubwa sana, najivunia na nina shukuru sana.” Umeeleza ujumbe huo, ulionukuu kauli ya Son.

Bosi wa Tottenham Jose Mourinho pia amempongeza Kane kwa ubora alikuwa nao katika mchezo huo kwa kuhusika katika mabao yote matano, huku ukiwa ushidni wa kwanza kwa Spurs msimu huu 2020-21, kufuatia kupoteza mchezo wa ufunguzi dhidi ya Everton.

Mbaroni kwa madai ya kumuozesha mwanafunzi
Shule kufunguliwa Oktoba mwaka huu - Uganda