Wapinzani wa Tanzania kwenye mbio za kufuzu AFCON 2017, Chad wamemteua nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya Cameroon, Rigobert Song kuwa kocha wao wa timu ya taifa.

Ripoti kutoka Chad zinasema shirikisho la mpira la nchi hio limemchagua mlinzi huyo wa zamani wa timu ya vilabu mbalimbali vya Ulaya ikiwemo Liverpool baada ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Emmanuel Tregoat kuachia ngazi.

Chad ilibamizwa na Misri mabao 5-1 kwenye mechi za Kundi G kufuzu kombe la Mataifa ya Afrika 2017 nchini Gabon.

Matokeo mabao zaidi kwenye mbio za kufuzu CHAN 2016 yalimweka vibaya zaidi kocha Tregoat na kuzua ripoti za Song kukabidhiwa mikoba yake mwezi uliopita.

Chad itakutana na Tanzania mwezi Machi kwenye mechi mbili mfululizo za nyumbani na ugenini za kusaka tiketi ya kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Gabon mwaka 2017.

Misri na Nigeria ni wapinzani wengne wa Tanzania kwenye Kundi hilo.

Song aliyeshinda kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2000 na 2002 anashikilia rekodi ya kucheza mechi nyingi zaidi kwenye mashindano hayo.

Matokeo Ubunge Mkoa Wa Singida, Lissu Na Kingu Wapata Majibu
Mkwasa Atangaza Kikosi Cha Taifa Stars