Hatimaye uongozi wa klabu ya Southampton, umefanikiwa kumpata mrithi wa kiungo Morgan Schneiderlin aliyetimkia Man Utd mwanzoni mwa juma hili kwa ada ya uhamisho wa paund 25.

Kiungo kutoka nchini Uholanzi Jordy Clasie, ndiye ameonekana kuwa chaguo sahihi katika uzibaji wa pengo la Schneiderlin na tayari amekamilisha kila hatua ya kujiunga na The Saint.

Clasie, amejiunga na Southampton akitokea nchini kwao Uholanzi alipokua akiitumikia klabu ya Feyenoord ambapo alikua nahodha wa kikosi cha klabu hiyo.

Ada ya usajili wa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24, imetajwa kuwa ni paund 8.4 ambazo ni sawa na Euro million 12.

Machali atimkia ACT- Wazalendo
Liverpool Yatangaza Jezi ya Robert de Oliveira Na Kikosi Chake