Viungo Dele Alli wa Tottenham Hotspurs na Jesse Lingard wa Manchester United, wameachwa kwenye timu ya taifa ya England, ambayo itacheza michezo miwili ya kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Ulaya (Euro 2020) dhidi ya Jamuhuri ya Czech na Bulgaria juma lijalo.

Kikosi cha England kitaanza kupambana dhidi ya Jamuhuri Ya Czechs Oktoba 11 na siku tatu baadae kutacheza dhidi ya Bulgaria.

Kocha mkuu wa kikosi cha England Gareth Southgate ametangaza kikosi chake na kufanya maamuzi ya kuwaita kwa mara ya kwanza wachezaji wa Chelsea Fikayo Tomori (beki) na Tammy Abraham (Mshambuliaji) huku kiungo wa Everton Fabian Delph akirejeshwa.

Kiungo wa mabingwa wa soka barani Ulaya Alex Oxlade-Chamberlain ameachwa sambamba na beki wa kulia wa Manchester United Aaron Wan-Bissaka ambaye ni majeruhi.

“Nimefanya mabadiliko kwa kuwaita wachezaji wengine, kutokana na sababu mbalimbali, lakini wengi wao ambao sikuwaita wanakabiliwa na majeraha ama viwango vyao kuwa katika hali ya kawaida,” alisema Southgate.

“Ninahitaji kuwa na wachezaji wenye dhima na uwezo wa kupambana, huku wengine tukiwapa wasaa wa kurekebisha kasoro walizonazo, ili tuwaite tena siku zijazo.”

Kikosi cha England kilichotajwa kwa ajili ya michezo ya kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Ulaya dhidi ya Jamuhuri ya Czech na Bulgaria.

Makipa: Tom Heaton (Aston Villa), Jordan Pickford (Everton) na Nick Pope (Burnley).

Mabeki: Trent Alexander-Arnold (Liverpool), Ben Chilwell (Leicester), Joe Gomez (Liverpool), Michael Keane (Everton), Harry Maguire (Manchester United), Tyrone Mings (Aston Villa), Danny Rose (Tottenham), Fikayo Tomori (Chelsea) na Kieran Trippier (Atletico Madrid).

Viungo: Ross Barkley (Chelsea), Fabian Delph (Everton), Jordan Henderson (Liverpool), James Maddison (Leicester), Mason Mount (Chelsea), Declan Rice (West Ham) na Harry Winks (Tottenham).

Washambuliaji: Tammy Abraham (Chelsea), Harry Kane (Tottenham), Marcus Rashford (Manchester United), Jadon Sancho (Borussia Dortmund), Raheem Sterling (Manchester City) na Callum Wilson (Bournemouth).

Tanzania: Wakimbizi 600 wa Burundi warudishwa kwao
Video: Serikali yashusha neema kwa wakulima, Mbolea bei chee