Katibu Mkuu wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Hassan Abbasi, amezitaka Kampuni za Ubashiri wa Michezo (Sports Betting) kuwa sehemu ya kuinua na kukuza michezo nchini.

Dk. Abbasi amesema hayo katika kikao alichofanya na Kampuni hizo ambapo amesema michezo ya kubashiri (Sports Betting) ina nafasi kubwa katika kuchangia maendeleo ya timu za Taifa hasa pale zinapokuwa katika mashindano.

 “Lengo la Serikali kwa sasa ni kuwekeza kimkakati kwenye michezo, tuwe na mpango wa moja kwa moja wa kuzisaidia timu zetu za Taifa kifedha, mimi naamini tukishirikiana kwa karibu tunaweza kuleta mabadiliko chanya katika sekta ya michezo” amesema Dk. Abbasi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Ubashiri wa Michezo Tanzania (TSBA), Jimmy Kenneth, ameiomba Serikali kutatua baadhi ya changamoto ikiwemo uwepo kwa kampuni za ubashiri ambazo hazina usajili nchini ambazo zinaisababishia nchi kukosa mapato, naye Dk. Abbasi ameahidi kulifanyia kazi suala hilo.

Atoka jela baada ya miaka 68, "Ilikuwa ni kama nimezaliwa upya"
ICC yamhukumu Ongwen kifungo cha miaka 25 jela