Uongozi wa klabu ya Tottenham Hotspur unaendelea na mazungumzo na Real Madrid ili kumrudisha nyumbani mshambuliaji wa pembeni kutoka Wales Gareth Bale.

Bale mwenye umri wa miaka 31, aliondoka Spurs na kujiunga na Real Madrid kwa ada ya usajili iliyoweka rekodi ya pauni milioni 85, mwaka 2013 na ameifungua klabu hiyo ya mjini Madrid mabao zaidi ya mabao 100 na kushinda mataji manne ya Ligi Mabingwa Barani Ulaya.

Akiwa Spurs, winga huyo alicheza zaidi ya mechi 200 kati ya 2007 na 2013, akifunga mabao 56 na assists 58 na wakala wake amesema kuwa atapenda kumrejesha Bale huko London.

“Gareth bado anaipenda Spurs. Ni mahali anapotaka kuwa” wakala wake Jonathan Barnett aliambia BBC.

Bale amekuwa akihusishwa na Manchester United lakini inaonekana Mashetani Wekundu bado watakosa kumsajili msimu huu wa joto.

Meneja wa Spurs, Jose Mourinho alisema kabla ya mechi yao ya kwanza waliyopoteza kwa bao 1-0 mbele ya Everton Jumapili kwamba alitaka klabu imsajili mshambuliaji kabla ya dirisha la uhamisho kufungwa Oktoba 5.

Huenda makubaliano ya mkopo yakafikiwa lakini changamoto ni mshahara wa mshambuliaji huyo, kwani anapokea karibu Pauni 600,000 kwa juma (Sawa na shilingi Bilioni 1.8 za kitanzania).

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Septemba 17, 2020
The Cranes: Rais Museveni timiza ahadi yako