Mchezaji Aaron Connolly wa timu Brighton alikuwa ni mwiba  mbele ya Tottenham Hotspur katika mchezo wa Ligi Kuu uingereza kwa kuwafunga mabao mawili wakati wakiibuka na ushindi wa mabao 3-0.

Bao la kwanza lilipachikwa na Neal Maupay dakika ya tatu na iliwabidi wasubiri mpaka dakika ya 32 kuandika bao la pili wakiwa nyumbani.

Mabao mawili ya ushindi yalifungwa dakika ya 32 na 65 yaliipoteza kabisa Tottenham kwenye reli na mfumania nyavu alikuwa ni Connoly.

Matokeo hayo yanaifanya Tottenham kuwa nafasi ya sita wakiwa na pointi 11 na wamecheza michezo nane.

Brighton inakuwa nafasi ya 13 ikiwa imecheza michezo nane na imekusanya pointi tisa.

Video: Rais Magufuli ampigia simu IGP Sirro, amuagiza kumsimamisha kazi kamanda wa polisi
Fahamu wanyama 10 wenye akili zaidi duniani