Uongozi wa Chama cha Wachezaji wa Soka nchini Tanzania (SPUTANZA), umeingilia kati suala la Beki kutoka nchini Ghana Lamine Moro na Uongozi wa klabu hiyo, linalohusishwa na utovu wa nidhamu.

Mwenyekiti wa SPUTANZA Mussa Kissoky amesema wamekua wakiliona suala hilo likisambaa katika mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari, lakini wanaamini mahala sahihi ya kulizungumza hilo ni mezani na wanaweza kumalizana kwa heri.

Kissoky ambaye kwa sasa anatetea nafasi yake kuelekea katika uchaguzi mku wa SPUTANZA, amesema wanaukaribisha Uongozi wa Young Africans na Lamine Moro mezani kujadili matatizo yao, na wanaamini yatakwisha salama.

“Nachukizwa sana na baadhi ya klabu wanavyoficha maovu ya wachezaji wanapoonyesha utovu wa nidhamu, hakuna mwana michezo duniani aliyefanikiwa bila kuwa na heshima, waache hiyo tabia ya kuangalia ukubwa au umaarufu wa mchezaji. 

“Halafu kuna suala limezuka kwa baadhi ya klabu mchezaji anapodai stahiki zake anaonekana hana nidhamu, naomba viongozi waangalie hili maana ni haki ya mchezaji kupata haki yake,” amesema Kisoky

SPUTANZA wameamua kuingilia kati suala hilo na kutangaza njia ambazo zinaweza kutatua mgogoro uliopo, baada ya mchezaji Lamine Moro kutoa malalamiko ya kuwa yeye hakuonyesha utovu wa nidhamu kwa viongozi wa benchi la ufundi.

Lamine anatuhumiwa kuonesha utovu wa nidhamu wakati kikosi cha Young Africans kilipokua kwenye maandalizi ya mchezo wa Ligi kuu dhidi ya Namungo FC uliochezwa mkoani Lindi mwezi uliopita.

Ajali ya treni yaua 30 Pakistani
CDU yashinda kwa kishindo katika jimbo la Saxony-Anhalt