Klabu ya Società Sportiva Calcio Napoli ya nchini Italia, imeonyesha dhamira ya kweli ya kutaka kukiongezea nguvu kikosi chake itakapofika mwezi januari mwaka 2016, baada ya kuwasilisha maombi ya kutaka kumsajili kwa mkopo mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid, Jese Rodriguez.

Uongozi wa Napoli umefikia hatua ya kuuliza jambo hilo, baada ya kuona mshambuliaji huyo hatumiki mara kwa mara kwenye kikosi cha Real Madrid msimu huu, na wanaamini huenda ikawa nafasi nzuri kwao kumsajili japo kwa mkopo ili kuona namna ya kutimiza lengo lake la kucheza kila juma.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 22, bado ana mkataba wa klabu ya Real Madrid mpaka mwezi June mwaka 2017.

Endapo Jese atakamilishiwa mpango wa kusajiliwa kwa mkopo na klabu ya SSC Napoli mwezi Januari mwaka 2016, atajiunga na mchezaji mwenzake aliyekua nae Real Madrid Jose Callejon.

Tanzania Mwenyeji Wa Kozi Ya Waamuzi Afrika
Ngebe, Majivuno, Tambo Kumalizwa Kesho Taifa Stadium