Msanii wa muziki wa Hip Pop, Boniventure Kabogo maarufu kama Stamina ambaye ameachia ngoma yake aliyoelezea stori ya kweli kuhusu kuvunjika kwa ndoa yake katika wimbo wake unaoenda kwa jina la Asiwaze aliyoimba na mwanamuziuki chipukizi Atan.

Roma ambaye ni rafiki wa karibu wa Stamina amesema alichoimba Stamina ni kisa cha ukweli kilichomtokea na yeye kama rafiki alitumia muda mwingi sana kuirudisha ndoa hiyo jambo ambalo liligongwa mwamba.

Mc pilipili ambae hivi karibuni alifunga ndoa alizungumza mtazamo wake kuhusu kuvunjika kwa ndoa hiyo ambapo amesema kuwa Stamina asiwajumuishe watu kwenye matatizo yake huku akigusia ndoa yake kuwa ipo vizuri na hategemei kama itakuja kuvunjika huku akijinadi kuwa anatamani angeoa miaka mitatu nyuma angekuwa na mafanikio ziaidi ya haya aliyoyapa.

”Stamina Sharobwenzi asitujumlishe sisi kwenye matatizo yake, matatizo yako ni matatizo yako binafsi,…na matatizo yake yamemfanya Stamina hadi leo awe mfupi, sisi tupo vizuri, mke wangu yupo poa miaka mitatu iliyopita ningekuwa vizuri zaidi” amesema Mc Pilipili.

Stamina alitumia ukurasa wake wa Instagrama kumjibu Mc Pilipili kama inavyosomeka hapa chini.

”Matatizo na Changamoto Ndani Ya Ndoa Yanaweza Kumkuta Mtu Yoyote Yule, Leo Ni Mimi Lakini Kesho Unaweza Ukawa Ni Wewe, Usijione Uko Salama Sana Ndani Ya Ndoa Yako Kaka (Weka Akiba Ya Maneno, Punguza Kejeli Na Dharau Utaheshimika Na Kupendwa Zaidi)
Usiharibu Na Kupoteza Sifa Na Heshima Uliyokuwa Nayo Kwa Kuzipaka Matope Ndoa Zingine Na Kuona Wewe Pekee Ndio Mwenye Ndoa Iliyo Imara!! Ipo Siku Utazipaka Matope Ndoa Na Harusi Unazozisimamia Kama MC Na Zitaharibu Biashara Yako Na Career Kwa Ujumla!! Unaongea Kwa Kujiamini Sana Kwamba Ndoa Yako Iko Salama Na Haiwezi Kuyumba, Na Unatuona Kama Sisi Wengine Hatuijui Ndoa Ila Ndoa Yako Tu Ndio Pekee iliyobarikiwa, Watu Wamekusikia Na Watatunza Maneno Yako Kama KumbuKumbu Na Muda Ndio Utaongea, MALIPO NI HAPAHAPA DUNIANI!!, Ubarikiwe Sana na kila la kheri katika ndoa yako🙏” ameandika Stamina.

Aidha katika wimbo huo Stamina ameonyesha kukasirishwa kwa kiwango kikubwa na aliyekuwa mke wake na katika mashairi ameimba kuwa, pete, mahali, mshenga, keki, sadaka ya ndoa hivyo vyote alifanya vya nini?.

Na moja ya mstari alioimba kwenye wimbo huo anasema mke wake akija kwenye msiba wake ataamka amchape vibao, zaidi hela atazopata afanye sherehe achome nyama ale na rafiki zake kwani yeye atazikwa na marafiki zake na mashabiki zake.

Kocha Mtibwa: Tuna deni kwa Simba
Atumia mwanasesele kama mtoto kuvusha vipodozi

Comments

comments