Timu ya soka ya Stand United ya Shinyanga ipo jijini Dar es salaam kwa ajili ya mchezo wa kesho wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga.

Mchezo huo utapigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam huku Stand ikitamba kufanya kweli na kuishangaza Yanga.

Msemaji wa Stand United, Deo Kaji Makomba alisema kikosi chao kipo kwenye hali nzuri kiafya kwa ajili ya mchezo huo.

Alisema wanajivunia mazoezi walioyapata pamoja na ukamilifu wa safu ya ushambuliaji inayoongozwa na Elias Maguli ambaye kwa sasa ni kinara wa mabao katika Ligi akiwa anaongoza kwa jumla ya magoli 9.

“Watu waje wajionee Stand jinsi inavyocheza kandanda la kuvutia”

Ni Wapi Jose Mourinho Atakapo Jistiri?
Game Ya Kihistoria Imechezwa Salama Wa Salmini Nchini Somalia