Katika hali ya kushangaza uongozi wa Klabu ya Stand United ya Shinyanga umesema hauna taarifa yoyote juu ya kuondoka kwa wachezaji wao Haruna Chanongo na Abuu Ubwa kwenda kufanya majaribio kwenye timu ya TP Mazembe ya Congo DR.

Hivi karibuni wachezaji hao walitimkia katika klabu hiyo ya Congo DR kwa ajili ya kufanya majaribio ya siku 10, zoezi ambalo walilifanya na hatimaye kufanikiwa kufuzu huku hivi sasa wakiwa wanasubiri kauli ya mwisho kutoka kwa mmiliki Moise Katumbi.

Lakini leo hii klabu ya Stand United imesema imekuwa ikisikia tu kwenye vyombo vya habari juu ya wachezaji hao lakini haina taarifa yoyote rasmi kuhusiana na kuondoka kwao.

Kushoto Haruna Chanongo akiwa na Abuu Ubwa nchini DRC wakifanyiwa majaribio TP MAzembe

Msemaji wa Stand United, Deo Kaji Makomba amesema kocha mkuu wa timu hiyo Patrick Liewig amemwambia kwamba katika meza yake hakuna taarifa yoyote juu ya kutokuwepo kwa wanandinga hao.

“Kocha Liewig amenidokeza kwamba anashangazwa na kitendo cha wachezaji hao(Chanongo na Ubwa) kutojitokeza mazoezini kwa kipindi kirefu, tena bila taarifa yoyote,”alisema Makomba.

Uongozi wa Stand unaonekana kuleta sintofahamu kwa sababu hivi karibuni wakala wa wachezaji hao alizungumza na vyombo vya habari na kukiri kwamba kila kitu kilikwenda sawa na kwamba waliwasiliana na uongozi wa Stand juu ya safari ya wachezaji hao.

Chris Smalling Amkubali Kinda Borthwick-Jackson Hadharani
Simba Washindwa Kumalizana Na Hemed Morocco