Kocha mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro, Charles Mkwasa amesema kikosi chake kipo tayari kwa mchezo wa kesho dhidi ya Malawi kuwania kufuzu kwa Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018.

Mkwasa amesema kikosi chake kipo kaika hali nzuri baada ya kufanya mazoezi ya mwisho leo asubuhi ambapo wachezaji wote wapo katika hali nzuri wakiwemo wachezaji wawili Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu kutoka klabu ya TP Mazembe ya Congo DR.

“Tunatambua umuhimu wa mchezo wa kesho, wachezaji wana ari na morali ya hali ya juu, kikubwa tunawaomba watanzania wajitokeze kwa wingi uwanjani kuja kutu sapoti katika mchezo huo wa kesho” Alisema Mkwasa.

Kwa upande wa kocha msaidizi wa Malawi (The Flames), Ramadhan Nsanzurwimo amesema wanaiheshimu Tanzania, wanatambua kesho kutakua na mchezo mzuri, na wao kama Malawi wamejiandaa vizuri kwa mchezo huo.

Mgombea Ubunge CCM Amsifia Lowassa
Yametimia! Mkwasa Bosi Wa Ukweli Kweli Stars