Afisa habari wa TFF, Baraka Kizuguto amesema mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Adi Yussuf anaechezea klabu ya Mansfield Town inayoshiriki ligi daraja la tatu nchiniUingereza hataungana tena na timu ya taifa baada ya  kupata majeraha wakati timu yake ilipocheza dhidi ya Nottingham Forest mwishoni mwa juma lililopita.
Uongozi wa klabu yake umemuomba kocha wa timu ya Taifa, Charles Boniface Mkwasa kumtomjumuisha kwenye kikosi cha timu ya taifa kwa sababu bado anaendelea kupata matibabu chini ya usimamizi wao.
Klabu hiyo imeahidi kuwa watamruhusu mchezaji huyo  kuitumikia timu ya Taifa baada ya kupata matibabu na kurejea tena uwanjani.

Vuguvugu La Usajili Barani Europa
Rodgers Amshangaa Dunga Wa Brazil