Meneja wa Taifa Stars, Nadir Haroub ‘Canavaro’ amesema timu itaingia kambini kesho katika hoteli ya Sea Scape jijjini Dar es salaam ambapo wachezaji wanaocheza soka la kulipwa nje ya nchi wataanza kuwasili kuanzia leo, na septemba 2, mwaka huu timu itaondoka kwenda nchini Burundi.

Cannavaro amesema baada ya kuingia kambini wataanza kufanya mazoezi katika uwanja wa Boko Veteran ambapo wachezaji wanaokipiga katika klabu za Simba na Yanga watajumuka na wenzao kambini baada ya michezo yao ya katikati ya wiki hii.

Kikosi cha wachezaji 30 kinachotarajiwa kuingia kambini  kinaundwa na makipa Juma Kaseja (KMC), Beno Kakolanya (Simba), Metacha Mnata (Yanga), mabeki ni Kelvin Yondani (Yanga), Erasto Nyoni (Simba), Boniface Maganga (KMC), Shomary Kapombe (Simba), Mohammed Hussein (Simba), Gadiel Michael (Simba), Iddi Moby (Polisi Tanzania) na Abdi Banda (Highlands- Afrika Kusini).

Kwa upande wa viungo wamo Hassan Dilunga, Jonas Mkude (Simba), Ally Ng’anzi (Mennesota-Marekani), Frank Domayo, Abubakar Salum (Azam Fc), Baraka Majogoro (Polisi Tanzania), Simon Msuva (Difaa El-Jadida-Morocco), Eliud Mpepo (Buildcon-Zambia), Mohammed Issa, Abdulaziz Makame (Yanga) na Farid Mussa (Tenerife-Hispania).

Na washambuliaji ni nahodha Mbwana Samatta (KRC Genk-Ubeligiji), Idd Nado, Shaaban Idd (Azam), Kelvin John (Mchezaji huru), Ayoub Lyanga (Coastal Union) na  Abdilahie Yussuf (Blackpool-England).

Stars itaanza mchezo wa kwanza ugenini mnamo Septemba 4,  2019 katika mtanange wa hatua ya awali ya kuwania kupangwa kwenye makundi ya kufuzu fainali za kombe la Dunia zitakazofanyika mwaka 2022 nchini Qatar ambapo itarudiana na Burundi septemba 8, 2019 mwaka huu kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Makonda aeleza sababu za yeye kuwa RC Dar
Serikali yapigilia Msumari Marufuku umiliki wa simu, Watoto chini ya miaka 18