Aliyekua beki wa kati wa timu ya taifa ya Uswiz pamoja na klabu ya Liverpool, Stephane Henchoz amekua mmoja kati ya wanaoendelea kumshambulia mshambuliaji mpya wa klabu ya Stoke City, Xherdan Shaqiri kufuatia uhamisho wake kutoka Inter Milan kuelekea nchini Engalnd kuhusishwa na tamaa ya fedha.

Henchoz, aliweka hadharani mtazamo wake alipokua akichambua mchezo wa kuwania kufuzu fainali za barani Ulaya za mwaka 2016 kati ya England ambao walikua nyumbani kwenye uwanja wa Wembley usiku wa kuamkia hii leo, dhidi ya timu ya taifa ya Uswiz ambayo ilikubali kufungwa mabao mawili kwa sifuri.

Henchoz, amesema anaamini uhamisho wa Shaqiri ulikua si wa mapenzi ya kucheza soka kama ilivyokua kwenye klabu nyingine na badala yake alitanguliza mbele tamaa ya mshahara mkubwa ambao umekua ukiwavuta wachezaji wengi kwenda kucheza ligi ya nchini England kwa sasa.

Beki huyo ambaye aliitumikia klabu ya Liverpool kuanzia mwaka 1999–2005, amesema Shaqiri tayari alikua ameshapata ofa kutoka kwenye klabu za nchini Ujarumania pamoja na Italia na ilionekana yu tayari kufanya maamuzi ya kucheza soka kati ya moja ya nchi hizo, lakini kwa mshangao mkubwa aligeuka na kufanya maamuzi ya kushangaza.

Shaqiri mwenye umri wa miaka 23, alikamilisha usajili wake wa paund million 12, wakati wa majira ya kiangazi baada ya meneja wa klabu ya Stoke City, Mark Hughes, kuthibitisha hadharani anavutiwa na kiwango cha mshambuliaji huyo.

Ester Bulaya Amuokoa Mtoto Wa Wasira Kuchomwa Moto
Samia Suluhu Atahadharisha Hujuma Dhidi Ya CCM