Klabu ya Dodoma Jiji imekamilisha usajili wa mshambuliaji wa zamani wa Namungo, Mghana Stephen Sey kwa ajili ya kuongeza nguvu huku ikitakiwa kuilipa Geita Gold kiasi cha Sh150,000, ikiwa ni nauli yake ya usafiri aliyopewa.

Sey alishindwana na Namungo katika dakika za mwishoni kwa kile kilichoelezwa kupandisha dau lake la usajili tofauti na lile walilokubaliana mwanzo, hivyo viongozi kuamua kuachana naye licha ya kupendekezwa na benchi la ufundi.

Wakati viongozi wa Namungo FC wakiachana na mpango huo, Geita Gold nayo ikajitosa kuhitaji saini ya Mghana huyo na rasmi alianza safari ya kwenda Geita ndipo akapokea simu ya mabosi wa Dodoma Jiji walioihitaji saini yake.

Nauli ya Mshambuliaji huyo kuelekea Geita ilitolewa na Uongozi wa Geita Gold ambapo walimpatia Shilingi 150,000 na alipofika njiani akabadili safari yake Baada ya kupigiwa Simu na kupewa ofa kubwa na Dosoma Jiji.

Kwa Mjibu wa watu wa Karibu wa Nyota huyo,Sey amepanga kurudisha Pesa hiyo Kwa viongozi wa Geita Gold FC.

Kocha Mubiru aishangaa Mbeya City
Ukame wazidi kuchochea dhuluma za kijinsia