Baada ya kushambuliwa na vyombo vya habari pamoja na mashabiki wa soka duniani kote kupitia mitandao ya kijamii, mshambuliaji kutoka nchini Uingereza, Raheem Sterling amesema hali ya ugonjwa ndiyo iliyomsambabisha kushindwa kufika kwenye mazoezi ya klabu ya Liverpool hapo jana.

Sterling, alidaiwa kutofika mazoezini ili kuushinikiza uongozi wa klabu ya Liverpool kuharakisha mchakato wa kuondoka kwake klabuni hapo, baada ya klabu ya Man City kuoyesha dhamira ya kweli ya kumsajili kwa paund milioni 40.

Mshambuliaji huyo ambaye amesaliwa na mkataba wa mwaka mmoja, amesema kutokufika kwake mazoezini hapo jana hakukutokana na maelezo yaliyotolewa na vyombo vya habari, bali alikuwa anasumbuliwa na maradhi ambayo hakuyaweka wazi.

Ilidaiwa kwamba Sterling, amekuwa akimshinikiza meneja wa klabu ya Liverpool, Brendan Rodgers, kutomjumuisha kwenye kikosi cha The Reds ambacho kitasafiri kuelekea nchini Australia pamoja na mashariki ya mbali kwa ajili ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi.

Singida Mjini Wamlilia Mo Dewji Baada Ya Kujiengua Ubunge
Van Persie Aendelea Kuandamwa Na Jinamizi Hili