Uongozi wa klabu ya Manchester City umekubaliana na Liverpool dili la kumsajili mshambuliaji kutoka Uingereza, Raheem Sterling.

Kwa mujibu wa kituo cha televisheni cha Sky Sports, viongozi wa klabu ya Man City imekubali dili hilo baada ya kuomba kupunguziwa ada ya uhamisho wa Sterling ambayo ilitajwa kuwa ni zaidi ya paund milioni 50.

Taarifa zinasema kwamba mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 20, atasajiliwa kwa ada ya uhamisho wa paund milioni 49.
Kiasi hicho cha pesa kitalipwa mara baada ya taratibu zote za uhamisho zitakapokamilika likiwepo suala la kupimwa afya kwa Sterling.

Peter Schmeichel Kufanya Kazi na Mwanae
Majambazi Wavamia Kituo Cha Polisi Ukonga Na Kufanya Mauaji