Kocha Mkuu wa Chelsea, Mauricio Pochettino amemtaka Raheem Sterling kuwa na muendelezo katika kiwango chake bora ili kumdhihirishia Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya England Gareth Southgate kuwa alikosea kumuweka nje ya kikosi chake.

Sterling alihusika katika mabao yote manne yaliyofungwa na Chelsea wakati ikiibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Burnley baada ya kuwa nyuma kabla ya kuibuka na ushindi.

Mkongwe huyo aliyecheza mechi 82 kwa mara ya mwisho aliichezea England katika fainali zilizopita za Kombe la Dunia na aliachwa nje ya kikosi mara nne mfukulizo katika mechi za kirafiki pamoja na Australia na mechi ya kufuzu kwa Euro 2024 dhidi ya Italia.

“Nafikiri kutokana na uzoefu wake najua anahitaji kucheza na kumuonesha kocha wa timu ya taifa kuwa alikosema kufanya uamuzi wake, “alisema Pochettino baada ya Chelsea kufunga mabao manne katika Ligi Kuu kwa mara ya kwanza tangu Aprili mwaka 2022.

“Kiwango na kufunga mabao ndio vitu pekee ambavyo vinaweza kuonesha kuwa mchezaji huyo bado anafaa kuwemo katika kikosi hicho cha taifa.”

Chelsea, wakiongozwa na Sterling, baadae walifunga mara tatu katika kipindi cha pili chenye nguvu na kuondoka na pointi zote tatu.

Sterling mshindi mara nne wa taji la Ligi Kuu, alishinda Penati baada ya kuchezewa faulo na beki Mbrazil Vitinho, ambayo ilisababisha Cole Palmer kufunga bao lake la kwanza kwa Blues tangu alipohamia akitokea Manchester City.

Mchezaji huyo wa zamani wa Mandhester City baadae alifungia timu yake bao la tatu.

Adre Mtine: Msitubeze, tutafuzu Robo Fainali
Biashara India, Tanzania kufanyika kwa Shilingi, Rupia