Wafanyabiashara wamepandwa na ghadhabu kubwa kutokana na matokeo ya kura ya maoni nchini Uingereza ambayo imeonesha wazi kuwa asilimia 52% ya Waingereza wangependa taifa hilo lijiondoe katika muungano wa EU.

Katika saa ya kwanza ya kuhesabu kura hiyo ya maoni, pauni ya Uingereza ilipanda na kuishinda dola ya Marekani, lakini kwa sasa imeshuka baada ya matokeo ya kura hiyo kuanza kuonyesha dalili ya Uingereza kujiondoa kutoka katika muungano wa mataifa ya bara Ulaya.

Thamani ya sarafu ya Uingereza, Sterling pound imeshuka kwa kiwango kikubwa mno kuwahi kutokea katika kipindi cha miaka 30 iliyopita.

Wafanyiabiashara wanasema kuwa hawajawahi kushuhudia mabadiliko makubwa ya kifedha kiasi hicho tangu wakati wa mdororo wa uchumi mwaka 2008.

Gavana wa benki kuu ya Uingereza kutoa mwelekeo kuhusiana na hatma hiyo

Masoko ya hisa katika mataifa ya bara Asia yameshuhudia pia mdororo kama huo huku Yen ya Japan ikishuka kwa thamani kubwa pia.

Thamani ya soko la hisa la Japan tayari limeshuka kwa asilimia 8.

Taasisi inayoratibu ubora wa soko na chumi wa mataifa Standard and Poor imeonya kuwa sasa Uingereza huenda ikapoteza ubora hadhi yake ya kuwa soko lenye uthabiti kuliko yote duniani ama ‘triple A rating’

Wadadisi wa maswala ya kiuchumi wanatabiri kuwa soko la hisa la Uingereza mjini London pia litaporomoka kufuatia kauli hiyo ya waingereza.

Gavana wa benki kuu ya Uingereza anatarajiwa kutoa mwelekeo muda mchache ujao kuhusiana na hali ya kiuchumi na sarafu ya Uingereza Sterling pound, katika muda mchache ujao.

Waziri Mkuu wa Uingereza atangaza kujiuzulu, Waingereza waamua kujiondoa EU
Video: Mbunge anataka kulipwa Milioni 243 alizotumia kuchimba visima 9