Mshambuliaji kutoka nchini Montenegro, Stevan Jovetic yu njiani kuihama klabu ya Man City baada ya mambo kumuendea kombo tangu aliposajiliwa akitokea nchini Italia kwenye klabu ya Fiorentina.

Jovetic, ambaye alisajiliwa kwa matarajio makubwa huko Etihad Stadium kutokana na kazi nzuri aliyokuwa akiifanya nchini Italia, anajiandaa kurejea tena nchini humo huku klabu ya Inter Milan inayonolewa na meneja Roberto Mancini, ikihusishwa kwa asilimia kubwa katika zoezi la kumsajili.

Baadhi ya vyombo vya habari mapema hii leo vimeripoti kwamba, mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25, anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya huko mjini Milan.

Uhakika wa vyombo hivyo vya habari kuripoti taarifa hizo, umepatikana kupitia tovuti ya klabu ya Inter Milan ambayo usiku wa kuamkia hii leo kugubikwa na taarifa kuwa ‘Jovetic atawasili kesho (leo) mjini Milan kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya afya.’

Jovetic, alijiunga na klabu ya Man City mwaka 2013 kwa usajili wa paund million 22, lakini mpaka anahusishwa na taarifa za kuondoka kwake mjini Manchester alikua amecheza michezo 43 na kufunga mabao 11.

Martinez Atamba Kuiletea Kombe Atletico Madrid
Walichosema Dr. Slaa, J. Makamba, Peter Msigwa, Kuhusu Lowassa kuhamia Chadema