Mshambuliaji wa klabu ya Liverpool, Daniel Sturridge ana matumaini makubwa ya kurejea uwanjani baada ya mwezi mmoja kuanzia sasa, kufuatia hali yake kiafya kuendelea vyema.

Sturridge ambaye alifanyiwa upasuaji wa pembozoni mwa japa (Hip) huko nchini Marekani mwishoni mwa mwaka jana, alitarajiwa kuwahi sehemu ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi kutokana na taarifa zilizokuwa zimetolewa hapo awali lakini mambo yamekuwa tofauti.

Kurejea kwake baada ya mwezi mmoja, kuinakadiriwa huenda akawa katika kikosi cha Liverpool kitakachoikabili Man Utd katika mchezo wa ligi ya Uingereza, ambao umepangwa kufanyika Septemba 12 mwaka huu.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25, ameizungumzia hali hiyo kwa kusema itakua ni jambo jema sana kwake kurejea uwanjani katika mchezo muhimu, na amewataka mashabiki wa Liverpool kumuombea ili malengo hayo yatimie.

Liverpool wanatarajia kuanza ligi ya msimu wa 2015-16, wakiwa na safu ya ushambuliaji ambayo itaongozwa na Christian Benteke, aliyesajiliwa mwezi uliopita akitokea Aston Villa.

Majaji Waliopokea Mgao Wa Escrow Kikaangoni
Profesa Lipumba: Sina Mpango Wa Kujiuzulu CUF, Lakini…