Mshambuliaji kutoka nchini Uruguay Luis Alberto Suárez Díaz ameshtumiwa na vyombo vya Uhamiaji nchini Italia kuwa aliingia kufanya mtihani wa Uraia akiwa na majibu.

Kwa mujibu Sky Italia wameripoti kuwa Suarez alikuwa katika mpango wa kupata uhamisho wa kujiunga na mabingwa wa soka nchini humo Juventus FC, na ilibidi kwanza afanye mtihani wa kawaida ili kujua uwezo wake katika kutumia lugha ya Kiitaliano ili aweze kukidhi kigezo cha kupewa hati ya kusafiria ya nchi hiyo (PASSPORT).

Kulingana na uchunguzi wa awali imebainika kuwa maswali yaliyokuwa katika mtihani huo tayari Suarez alikuwa ameyapita mapema na ndipo alipotiliwa shaka kwani hawezi kuongea neno lolote la Kiitaliano.

Mabingwa wa soka Italia Juventus FC tayari walikua wamekamilisha nafasi za wachezaji wa kigeni ambao hawatoki katika mataifa ya Umoja wa Ulaya kwa msimu huu, na mshambuoiaji huyo mwenye umri wa miaka 33 angesajiliwa naklabu hiyo endapo angepata uraia wa Italia.

Ripoti zinadai pande zote mbili zilikuwa tayari zimekamilisha makubaliano binafsi, lakini dili hilo halikuweza kufanikiwa kwa sababu ya uraia.

Hata hivyo jana Jumanne, Septemba 22 Suarez ameripotiwa kurejea nchini Hispania na huenda akajiunga na Atletico Madrid, baada ya kuwa sehemu ya wachezaji wanaoachwa na FC Barcelona, kufuatia kutokua sehemu ya mipango ya meneja mpya wa klabu hiyo Ronald Koeman.

Suarez aliyejiunga na FC Barcelona akitokea kwa mabingwa wa England liverpool FC mwaka 2014, na anaondoka Camp Nou akiwa amefunga mabao 147 katika michezo 191 aliyocheza.

Vifo vya covid-19 vyaishangaza Marekani, mara 67 ya shambulizi la Al-Qaeda
Guterres aingilia kati 'vita' ya Marekani na China