Nchi za Sudan kusini na Comoro zimekata tiketi ya kucheza hatua ya makundi ya kuwania kufuzu fainali za Afrika za 2019 ambazo zitachezwa Cameroon.
Nchi hizo zimekata tiketi na kuwa miongoni mwa zile zitakazowania nafasi 15 za kufuzu, baada ya kupata matokeo ya jumla katika michezo miwili ya nyumbani na ugenini.
Sudan kusini imeibomoa Djibouti mabao sita kwa sifuri katika mchezo wa mkondo wa pili uliocheza mjini Juba, baada ya kuambulia kisago cha mabao mawili kwa sifuri kwenye mpambano wa mkondo wa kwanza uliochezwa mjini Djibouti, mwishoni mwa juma lililopita.
Sudani Kusini imesonga mbele kwenye hatua ya makundi kwa jumla ya ushindi wa mabao sita kwa mawili.
Taifa hilo changa katika medani ya soka barani Afrika, linaingia moja kwa moja katika kundi C lenye timu za Mali, Gabon and Burundi.
Mchezo mwingine wa kuwania kufuzu hatua ya makundi ya AFCON 2019 ulikua kati ya Mauritius dhidi ya Comoro, ambao ulimalizika kwa sare ya bao moja kwa moja.
Matokeo hayo yanaipa nafasi Comoro kupata ushindi wa jumla wa mabao matatu kwa moja.
Katika mchezo wa mkondo wa kwanza Comoro walipata ushindi wa mabao mawili kwa sifuri.
Comoro wamefaulu na kutinga katika kundi B lenye timu za Malawi, Morocco pamoja na mabingwa watetezi Cameroon.
Baada ya kukamilika kwa michezo ya mtoano, makundi ya kuwania kufuzu fainali za AFCON 2019 yamekamilika.
A: Senegal, Equatorial Guinea, Sudan, Madagascar
B: Cameroon, Morocco, Malawi, Comoros
C: Mali, Gabon, Burundi, South Sudan
D: Algeria, Togo, Benin, The Gambia
E: Nigeria, South Africa, Libya, Seychelles
F: Ghana, Ethiopia, Sierra Leone, Kenya
G: DR Congo, Congo, Zimbabwe, Liberia
H: Ivory Coast, Guinea, Central African Republic, Rwanda
I: Burkina Faso, Angola, Botswana, Mauritania
J: Tunisia, Egypt, Niger, Swaziland
K: Zambia, Mozambique, Guinea-Bissau, Namibia
L: Cape Verde, Uganda, Tanzania, Lesotho