Serikali ya Sudan Kusini imependekeza mswada wa sheria wa kurefusha kipindi cha urais cha Rais, Salva Kirr kwa miaka mitatu, hatua inayoweka hatarini mazungumzo ya amani kati ya serikali na wapinzani.
Mswaada huo utalazimisha marekebisho ya katiba ili kuongeza muhula wa Rais Kiir hadi mwaka 2021 atakapomaliza muda wake.
Aidha msemaji wa kundi la waasi la Riek Machar, Lam Paul Gabriel, amesema kuwa serikali inapendekeza hatua ambayo ni kinyume cha sheria ya kujaribu kuongeza muhula wa Rais Kiir madarakani.
Machar walikutana na kutia saini makubaliano mapya ya amani yaliyojumuisha kusitisha mapigano, makubaliano ambayo yalitakiwa kuanza kutekelezwa siku ya Jumamosi.
Hata hivyo, makubaliano hayo yalivunjwa siku hiyo hiyo baada ya vikosi vya serikali na waasi kuanza kushambuliana.
-
Serikali ya Sudani yalaumiana na waasi wa nchi hiyo
-
Waziri ang’aka taarifa za kukatika ‘ziwa’ kwenye bomu lililomlenga Rais
-
Mfungwa atoroshwa kibabe mbele ya walinzi wa gereza