Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir amelivunja Bunge na atateua Wabunge wapya kutoka pande mbili zilizokuwa na mzozo ili kutekeleza Makubaliano ya Amani yaliyotiwa saini kumaliza mzozo uliozua vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Mzozo wa Sudan Kusini ulianza mwaka 2013 baada ya Rais Kiir, kutoka jamii ya Wadinka kumfukuza kazi Makamu wake, Riek Machar kutoka Kabila la Nuer.

Licha ya kufikia makubaliano, mapigano bado yanaendelea katika baadhi ya maeneo.

Makubaliano ya Amani yanataka kuongezwa kwa idadi ya wabunge, kutoka 400 wa hivi sasa hadi kufikia 550, na lazima Bunge hilo lihusishe watu kutoka pande zote mbili zilizokuwa katika mzozo.

Waliotoka jela kwa msamaha wa Rais Samia wauawa
Serikali yaingilia kati kuahirishwa mechi Simba na Yanga