Uongozi wa upinzani nchini Sudan kusini umekataa mapendekezo ya utawala wa mpito wa kijeshi uliopendekeza kufanyika kwa mazungumzo mapya baina yake na Upinzani siku ya jana, ikiwa ni siku mbili baada ya kuvamia kambi za waandamanaji.
Mvutano huo umetokea baada ya mabishano ya muda mrefu kati ya upinzani na jeshi kuhusu nani aongoze nchi ya Sudan katika kipindi cha mpito walichonacho baada ya kumng’oa madarakani aliyekuwa Rais, Omar Al-Bashir.
Kwa mujibu wa madaktari walio na uhusiano wa karibu na upinzani wamedai vifo vya watu kutokana na operesheni ya jeshi iliyofanywa kuanzia jumatatu vimeongezeka na kufikia 108 huku hofu ya kuongezeka ikitawala.
Katika taarifa yao wamesema kuwa miongoni mwa waliokufa, miili 40 iliopolewa katika mto nile na inadaiwa kuwa vikosi vya jeshi viliificha ili kupunguza idadi ya watu waliouawa katika vurugu hizo.
Hata hivyo shirika la habari la taifa hilo, SUNA mapema leo limesema kuwa kwa mujibu wa wizara ya Afya nchini humo idadi ya vifo vilivyo thibitishwa ni 46 tu.