Serikali ya Sudan imeripoti kutokea kwa jaribio la mapinduzi lililotokea katika nchi hiyo na hatua zilizochukuliwa kudhibiti hali hiyo ambapo vyombo vya habari vya serikali vimeripoti.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ufaransa (AFP) limesema kuwa jaribio hilo liliambatana na mpango wa kutwaa jengo ambalo linatumiwa pia na Shirika la Utangazaji la Sudan lililopo katika Mji wa Khartoum.

Msemaji wa Serikali aliyenukuliwa na mashirika ya habari ya kimataifa amesema wapangaji wa mapinduzi walijaribu kuchukua udhibiti wa redio ya Serikali huko Omdurman, ng’ambo ya mto Nile kutoka mji mkuu Khartoum.

Amesema Maandamano yalikuwa yamepangwa kufanyika mjini Khartoum leo na wanajeshi walikuwa wametumwa kushika doria mitaani wakati mapinduzi hayo yalipojaribiwa.

Serikali ya mpito ya Sudan ambayo imekuwepo tangu 2019 imekuwa ikikabiliwa na shinikizo la kuleta mageuzi ya kiuchumi na kisiasa licha ya madai yanayokinzana kutoka kwa maeneo ya kihafidhina na yale huria.

Mkuu wa Mkoa Singida atoa maagizo kwa MA-DC na Wakurugenzi
Wananchi msidharau mabadiliko tabia ya nchi - Rais Samia