Katibu wa baraza la mawaziri nchini Japan  ,Yoshihide Suga anatarajia kuzunguza na vyombo vya habari kuhusu uchaguzi wa  mrithi wa  waziri mkuu  Shinzo Abe ambaye pia ndiye kiongozi wa chama cha  Liberal Democratic Party (LDP).

Suga anahitisha mkutano na vyombo vya habari kwa lengo la kuthibitisha mpango wake kuwania nafasi hiyo.

Msaidizi huyo wa muda mrefu wa waziri mkuu Abe, amekuwa akitajwa kuwa kwenye nafasi nzuri ya kushika nafasi ya kuongoza chama cha LDP  na waziri mkuu wa taifa hilo .

Wiki moja iliyopita Abe alitangaza maamuzi yake ya kujiuzulu kutokana na matatizo ya kiafya.

Suga anakabiriwa na upinzani mkali toka kwa aliekuwa waziri wa ulinzi, Shigeru Ishiba, na waziri mstaafu wa mambo ya kigeni Fumio Kishida,

DCPC : Mbowe awaombe radhi TBC
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Septemba 2, 2020

Comments

comments