Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph ‘Sugu’ Mbilinyi amepongeza kazi inayofanywa na Wizara ya Maliasili na Utalii katika kutangaza vivutio vya utalii.

Sugu ametoa sifa hizo alipokuwa anachangia bungeni mjadala wa bajeti ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020.

“Napenda kuipongeza wizara kwa ile branding ya Tanzania Unforgettable. It’s a super thing (ni kitu kikubwa/kizuri), nilipoiona ile tu nikajua sasa Kigwangalla yuko kazini,” alisema Sugu ambapo picha za video zilimuonesha waziri wa Wizara hiyo, Hamisi Kigwangalla akimpa saluti.

Hata hivyo, pongezi za Sugu ziliambatana na ushauri wa kuboresha zaidi utangazaji wa sekta ya utalii katika anga za kimataifa.

“Lakini ipeleke kimataifa, CNN, BBC na kwenye platform nyingine za kimataifa. Na wewe brother (kaka) safiri. Nenda Ulaya, nenda Marekani ukajue watalii wanataka nini ili uje uwaandalie hayo mazingira huku,” alisema.

Mbunge huyo wa Mbeya Mjini pia alisema kuwa maagizo ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuhusu kuondolewa kwa tozo mbalimbali katika biashara litekelezwe haraka kwenye mahoteli ya kitalii ili wawekezaji katika sekta hiyo wapate unafuu wa kuboresha huduma ili kuwavutia zaidi watalii.

Messi azungumzia maumivu ya kipigo cha Liverpool
Lugola awatumbua askari sakata la mahabusu kutoroka