Siku chache baada ya Mr. Blue kuanzisha tafrani kwenye mitandao ya kijamii akimtuhumu Sugu kwa kupora wimbo wake wa ‘Freedom’ aliofanya naye awali, rapa huyo nguli amemualika kwenye kampeni ya wimbo huo.
Sugu ametoa wito wake kwa wasanii wote akiwemo Mr. Blu kutumia mdundo wa wimbo huo kurekodi wimbo wa Freedom kwa namna wanavyoona inawapasa ikiwa ni sehemu ya kampeni maalum ya ‘Freedom’.
Mualiko wa Sugu kwa Mr. Blue ulikuja dakika chache baada ya nguli hiyo wa muziki nchini aliyekuwa ameongozana na timu nzimba ya MJ Records katika kipindi cha Friday Night Live cha East Africa TV, kutoa ufafanuzi kuhusu uhalisia wa umilki wa wimbo huo.
Master Jay, Marco Chali na Daxo Chali (producer wa Freedom) walimsindikiza Sugu katika kipindi hicho na kutolea ufafanuzi wimbo huo.
Daxo Chali alieleza kuwa wimbo huo ni mali yake kwani alitengeneza mdundo na kibwagizo alichompa msanii wake, kisha akampa idea Mr Blue na Sugu ambao walifanya wimbo wa kwanza. Mtayarishaji huyo amedai kuwa baada ya version ya kwanza kukamilika huku Mr Blue akiishia kuiweka kwenye mtandao wa Mkito na YouTube, Sugu aliomba kufanya version yake na aliruhusiwa.
Jana, Sugu alitambulisha rasmi video ya wimbo huo kwenye kipindi cha Friday Night Live. Video imeongozwa na Hanscana.