Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi akizungumza bungeni leo Juni 20, 2018 amesema atatumia mawakili sita kulifungulia mashtaka Baraza la sanaa la Taifa (BASATA) kupinga kufungiwa wimbo wake wa #219.

Sugu amesema kuwa siku hizi kila Taasisi imegeuka kuwa polisi ikiwemo Basata walioufungia wimbo wake uliovuja kabla ya kutolewa rasmi na kudai kuwa Basata imefungia wimbo huo bila kujua gharama alizotumia kuutengeneza.

”Wimbo umevuja wao wanatoa statement (taarifa) ya kuufungia. Hawajawahi hata kuingia studio, hawajui hata gharama. Wanataka wote tuimbe nyimbo za mapenzi,” amehoji Sugu.

Hata hivyo Naibu Waziri wa Habari, Juliana Shonza amekanusha kile kilichokuwa kinazungumzwa na Sugu akidai kuwa wimbo huo tayari umetoka na mashairi yake anayo.

”Wimbo unavuja vipi wakati uko kwenye mitandao. Hata mashairi yake ninayo hapa. Nyie wenyewe mlisema Basata wanafungia nyimbo bila taarifa’ Shonza.

Baada ya Taarifa hiyo Sugu aliongezea kwa kusema ” Mimi sio kama Roma, Naiburuza Mahakamani Basata wimbo umevuja mimi sijautoa bado. Nina mawakili sita nitawaburuza mahakamani ndio watakoma”.

Aidha Taarifa ya Basata inasema imefikia maamuzi hayo ya kuufungia wimbo huo mara baada ya kuona una maneno ya uchochezi na kuhatarisha amani na utangamano miongoni mwa jamii, Pia Basata imetoa onyo kwa Sugu kuusambaza wimbo huo kwa watu wengine.

 

 

Video: Mashabiki wa rapa aliyeuawa wafunga mitaa kwa fujo
Mouez Hassen aondolewa kikosini